Saturday, 25 February 2017

MSAADA WA MATIBABU KWA MTOTO.

Anaitwa CLINIUS TUSHABE COSMAS

Alizaliwa mwaka 2007, mkoani  Kagera, wilaya ya Muleba kijiji cha Kitoko. Mtoto huyu ni YATIMA amefiwa na wazazi wote wawili na kwa sasa analelewa na mjomba wake asie na kazi maalum zaidi ya kufanya vibarua ili apate pesa za matumizi.

Mtoto huyu alipata ajali ya kuanguka kwenye mti mwaka 2013 na kuvunjika mguu unaoonekana picha , mguu huo uluivunjika sehemu ya goti na kusababisha mfupa kutoka nje na kuonekana.

Baada ya kupata ajali hiyo alipelekwa Zahanati ya kijiji ambako walishindwa kumpa matibabu na kushauri apelekwe Hospitali za Rufaa ili aonane na mabingwa wa mifupa. Tangu mwaka huo mpaka leo hajapatiwa tiba yoyote, hali hiyo imesababisha mguu huo kuanza kuvia kwa ndani na unampa maumivu makali sana.

Mwaka huu amejitokeza msamaeria mwema anaitwa mwalimu JAMES alifanikiwa kumpeleka Hospitali ya misheni kwa uchunguzi ambako madaktari wamesemea anaweza kupona kwa kufanyiwa operesheni kubwa ya mguu.

HIVYO UKIWA KAMA MDAU UNAOMBWA CHANGO WAKO WA HALI NA MALI ILI KUMSAIDIA MTOTO HUYU AREJEE KWENYE HALI YAKE YA KAWAIDA NA AWEZE KUENDELEA NA MASOMO.

KWA MAELEZO ZAIDI UNAWEZA KUWASILIANA NA MWALIMU ANAYEMUHUDUMIA ANAITWA MWALIMU JAMES NAMBA 0786 511 431

AU MWALIMU ELIZA NAMBA 0717 049 912 (KWA SMS TU) AU 0752 737 275 (KWA SMS TU)

KUTOA NI MOYO.    TUNATANGULIZA SHUKRANI ZA DHATI.



.

Monday, 31 October 2016

MOMBO TOUR

                      

                                                                     AMIRI  ALLY.
                                                           

Anaitwa Amiri Ally,ana umri wa miaka 16,anaishi kitongoji kinachoitwa "mwisho wa shamba"kilichopo Mombo , wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
Chanzo  cha ulemavu:
Hakuna maelezo ya kitaalamu zaidi yanayoeleza kwa undani chanzo cha ulemavu wake,lakini mama yake amesema kuwa alipata homa kali ya Malaria akiwa na ujauzito hali ilyopelekea kujifungua mtoto akiwa mdogo na mwenye uzito mdogo sana na kupata ulemavu wa akili kadiri alivyokuwa akikua.
Amiri Ally ni mlemavu wa viungo na akili anaehitaji msaada  wa hali na mali hasa kupata baiskeli ya walemavu, kwa sababu baiskeli hii itamsaidia:
1.Kuhudhuria shuleni bila kukosa (umbali wa kutoka nyumbani mpaka shuleni ni takribani kilometa 5).
2.Kushirikiana na watoto wenzake katika michezo na hivyo kuongeza uwezo wa akili yake na kukuza mawasiliano.

His name is Amiri Ally aged 16 years old, he lives at a place called " Mwisho wa Shamba ", Mombo, Korogwe District, Tanga Region.

The source of Disability :
There is no more details of the reviews that describe about source of his disability, but his mother says that during her pregnancy, she developed a high fever of Malaria whchi caused her to give birth  child with low weight.
The situation has prompted Amiri Ally born with mental  retardation and physical disabilities as he grew up.

Amiri Ally isa mental disabled who needs material and moral  support especially wheelchair, he needs a wheelchair because will help:
1. Attending school without missing (The distance from home to school is approximately 5 kms)
2. Playing with other children, improving his mental abilities and proper communication.


Mweka hazina wa NAPD TANZANIA  bi Blandina Hiza Malale akifurahia jambo na mtoto Amiri Ally wakati wa ziara ya kumtembelea nyumbani kwao Mombo.

NAPD TANZANIA chief accountancy Mrs Blandina Hizza Malale enjoying a chit chat with Amiri Ally during a home visit at Mombo.



Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya NAPD TANZANIA bi Bahati Mussa Abdi na Bw Jackson Tarimo wakifurahia jambo na mtoto Amiri Ally wakati wa ziara ya kumtembelea nyumbani kwao Mombo.

NAPD TANZANIA members of the Board of Directors Mrs Bahati Musa Abdi and Mr Jackson Tarimo enjoying a chit - chat with Amiri Ally during a home visit at Mombo.




NAPD TEAM MEMBERS.


Mtoto Amiri Ally anahitaji msaada wako wa hali na mali ili kumuwezesha kutimiza ndoto zake, kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na NAPD TANZANIA.
                          e mail  : napdtz2016@gmail.com
                           phone : +255 752 737 572 (sms tu)
                                       +255 71 7 978 281

Amiri Ally needs your help to enable him fulfill his dreams, for more information please contact :
                          e mail : napdtz2016@gmail.com
                          phone : +255 752 737 572
                                      +255 717 978 281

Friday, 28 October 2016

SOMANDA A MKOANI SIMIYU

Mwalimu Alex Benson akiwa katika viwanja vya kitengo cha Somanda A mkoani Simiyu
Mwl Elisha Maduhu ambae ni mtaalamu wa Elimu maalum fania ya Ulemavu wa akili akiwa Chuo cha Elimu maalum Patandi.
Wanafunzi wa kitengo cha walemavu wa akili na Viziw wakiwa katika picha ya pamoja kitengo cha Somanda kilichopo mkoani Simiyu

KITENGO CHA CHUDA

Mweka hazina wa NAPD  bi Blandina Hizza ambae kitaluma ni mwalimu wa walemavu fani ya viziwi akiwa darasani na wanafunzi wake wa darasa la V. Walemavu wakiwezeshwa wanaweza.
Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya NAPD bw Amani Kabelwa ambae kitaaluma ni mwalimu wa walemavu fani ya viziwi akiwa darasani na wanafunzi wake wa darasa la VI ambao wanatarajia kuingia la VII mwakani

Sadath, ni mwanafunzi wa kitengo cha ulemavu wa akili CHUDA akiwa amepumzika baada ya masomo



Friday, 21 October 2016

ULEMAVU NA WALEMAVU.


 Kuna maandiko mbalimbali yanayoeleza kwa mapana zaidi dhana ya Ulemavu,kila moja inajitosheleza na ina mapungufu yake.Kwa hali hiyo basi nami nimekuja na dhana yangu kulingana na uzoefu wangu kuhusu makundi mbalimbali ya walemavu.
Ulemavu ni hali inayotokana na dosari ya kimwili,kiakilina kimaono ya muda mfupi au ya kudumu.
Idadi ya waleamvu Duniani ni kubwa sana kuliko watu wengi wanavyofikiri,hasa watoto wanaozaliwa makubwa zaidi.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeelezea kuwa 10% ya watoto Duniani wana Ulemavu wa aina mbalimbali. Matokeo ya utafiti wa watu wenye ulemavu (Youth with Disabilities Project – 2007) yanaonyesha kwamba asilimia 5 ya watoto nchini Tanzania wana ulemavu wa aina mbalimbali.
Hii ina maana kuwa kila watoto 100 wanaozaliwa, 5 wana ulemavu wa aina mbalimbali.
Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002 ilibainisha kuwa asilimia mbili ya watu wote waliohesabiwa wana ulemavu wa aina mbalimbali. Hivyo basi jumla ya watu 3,456,900 walikuwa ni walemavu kwa kipindi cha sensa hiyo.
Katika sensa hiyo, baadhi ya makundi ya walemavu yalikuwa kama ifuatavyo:
1.      967,932  =  28% - Walemavu wa viungo.
2.      933,363  =  27%  - Walemavu wa kuona
3.      691,380  =  20%  - walemavu wa kusikia
Mbali na hayo, takribani watoto 350,000 wenye umri wa kwenda shule miaka 7 – 13 wana ulemavu.
Takwimu hizo hapo juu zinadhihirisha umuhimu wa Elimu maalum kwa jamii.Nitaelezea kwa kifupi dhana ya Elimu Maalum.
Elimu Maalum ni taaluma anuai inayotolewa kwa watu wenye mahitaji maalum kwa lengo la kuwawezesha watu hao kutimiza malengo yao ya msingi.
Malengo hayo hutofautiana kutokana na mahitaji ya msingi ya kundi husika, kwa mfano malengo ya Elimu maalum kwa watoto wenye ulemavu wa akili ni tofauti na malengo ya Elimu maalum kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia na kuona.
Elimu maalum ni taaluma ambayo mtu husoma kwa kipindi maalum na hugawanyika katika fani kuu tatu,ambazo ni:
1.      Fani ya ulemavu wa kusikia
2.      Fani ya ulemavu wa kuona
3.       Fani ya ulemavu wa akili
Fani zote hizi tatu zinafundishwa hapa nchini kwenye vyuo mbalimbali kama Patandi – Arusha ( ndio chuo cha kwanza kwa Elimu maalum nchini) , vingine ni SEKOMU – Lushoto na UDOM – Dodoma.
Makala ijayo nitaeleza kwa kina mlemavu wa kusikia ni nani, anajifunzaje, Vikwazo anavyokutana navyo na namna gani jamii inaweza kumsaidia mlemavu huyu kutimiza malengo yake.
Nakaribisha mjadala kwa makala hizi.
Ibrahim Ayubu
Mwenyekti – NAPD TANZANIA
Mob: 0652 040903 (sms tu)

kitengo cha viziwi Chuda






Wanafunzi kitengo cha Viziwi Chuda wakifurahia chakula chao cha mchana kinachotolewa shuleni hapo
                                

wazazi wa wanafunzi wa kitengo cha viziwi Chuda wakiwa kwenye kikao cha kujadili maendeleo ya watoto wao.           

Monday, 17 October 2016

NAPD TANZANIA - SIKU YA VIZIWI DUNIANI

MAADHIMISHO YA WIKI YA VIZIWI DUNIANI
Ushiriki wa wazazi na wanafunzi katika usafi Hospitali ya Bombo

Wanafunzi wa shule ya msingi Chuda kitengo cha viziwi na wa shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga pia walikuwa ni sehemu ya jamii walioshiriki usafi katika hospital ya Rufaa Bombo.




Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya NAPD Jackson Tarimo akishiriki kufanya usafi katika hospitali rufaa ya Bombo kama sehemu ya kuadhimisha wiki ya viziwi Duniani




Mwenyekiti wa NAPD bwana Ibrahim Ayubu katikati akiwa na mweka hazina wa NAPD bi Blandina Hizza kulia, na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya NAPD bwana Amani Kabelwa kushoto,wakijiandaa kutoa maelekezo kuhusu upimaji wa masikio wakati wa Maadhimisho ya wiki ya viziwi Duniani

Mkuu wa kitengo cha watoto viziwi Chuda mwalimu Beatrice Amiri akitoa maelezo juu ya hatua za kufuata kabla , wakati na baada ya kumpima mtoto usikivu kwa kutumia mashine maalum mbele ya mgeni rasmi , katibu tawala wa mkoa wa Tanga
Mwenyekiti wa CHAVITA TAIFA bwana Nidrosy Mlawa akifafanua jambo mbele ya mgeni rasmi, katibu tawala wa mkoa wa Tanga,kulia alieshika maiki ni mkalimani