Kuna maandiko mbalimbali yanayoeleza kwa
mapana zaidi dhana ya Ulemavu,kila moja inajitosheleza na ina mapungufu
yake.Kwa hali hiyo basi nami nimekuja na dhana yangu kulingana na uzoefu wangu
kuhusu makundi mbalimbali ya walemavu.
Ulemavu ni hali inayotokana na dosari ya kimwili,kiakilina kimaono ya
muda mfupi au ya kudumu.
Idadi ya waleamvu Duniani ni kubwa
sana kuliko watu wengi wanavyofikiri,hasa watoto wanaozaliwa makubwa zaidi.
Shirika la Afya Duniani (WHO)
limeelezea kuwa 10% ya watoto Duniani wana Ulemavu wa aina mbalimbali. Matokeo
ya utafiti wa watu wenye ulemavu (Youth with Disabilities Project – 2007)
yanaonyesha kwamba asilimia 5 ya watoto nchini Tanzania wana ulemavu wa aina
mbalimbali.
Hii ina maana kuwa kila watoto 100
wanaozaliwa, 5 wana ulemavu wa aina mbalimbali.
Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002
ilibainisha kuwa asilimia mbili ya watu wote waliohesabiwa wana ulemavu wa aina
mbalimbali. Hivyo basi jumla ya watu 3,456,900 walikuwa ni walemavu kwa kipindi
cha sensa hiyo.
Katika sensa hiyo, baadhi ya makundi
ya walemavu yalikuwa kama ifuatavyo:
1. 967,932 = 28%
- Walemavu wa viungo.
2. 933,363 =
27% - Walemavu wa kuona
3. 691,380 =
20% - walemavu wa kusikia
Mbali na hayo, takribani watoto
350,000 wenye umri wa kwenda shule miaka 7 – 13 wana ulemavu.
Takwimu hizo hapo juu zinadhihirisha
umuhimu wa Elimu maalum kwa jamii.Nitaelezea kwa kifupi dhana ya Elimu Maalum.
Elimu Maalum ni taaluma anuai inayotolewa kwa watu wenye mahitaji maalum
kwa lengo la kuwawezesha watu hao kutimiza malengo yao ya msingi.
Malengo hayo hutofautiana kutokana na
mahitaji ya msingi ya kundi husika, kwa mfano malengo ya Elimu maalum kwa
watoto wenye ulemavu wa akili ni tofauti na malengo ya Elimu maalum kwa watoto
wenye ulemavu wa kusikia na kuona.
Elimu maalum ni taaluma ambayo mtu
husoma kwa kipindi maalum na hugawanyika katika fani kuu tatu,ambazo ni:
1. Fani ya ulemavu wa kusikia
2. Fani ya ulemavu wa kuona
3. Fani ya ulemavu wa akili
Fani zote hizi tatu zinafundishwa
hapa nchini kwenye vyuo mbalimbali kama Patandi – Arusha ( ndio chuo cha kwanza
kwa Elimu maalum nchini) , vingine ni SEKOMU – Lushoto na UDOM – Dodoma.
Makala ijayo nitaeleza kwa kina
mlemavu wa kusikia ni nani, anajifunzaje, Vikwazo anavyokutana navyo na namna
gani jamii inaweza kumsaidia mlemavu huyu kutimiza malengo yake.
Nakaribisha mjadala kwa makala hizi.
Ibrahim Ayubu
Mwenyekti – NAPD TANZANIA
Mob: 0652 040903 (sms tu)
No comments:
Post a Comment